Jumamosi , 8th Aug , 2020

Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu amekabidhiwa fomu za kuwania nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020 na Tume ya na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Lissu akiwa na mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu

Akimkabidhi fomu hizo mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Kaijage amesema kuwa uteuzi utafanyika Agosti 25 na wagombea watatakiwa kurejesha fomu hizo kwa wakati ili tume iweze kupitia na kufanya uteuzi kwa waliokidhi vigezo.

“Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na sharia ya uchaguzi, ikijiridhisha mnayo sifa mtateuliwa”, amesema Jaji Kaijage.

Mpaka sasa vyama ambavyo vimeshachukua fomu ili kuwania nafasi hiyo ni Chama Cha Demokrasia Makini, AAFP, NRA, CCM, DP, UDP, ADC, SAU, ACT-Wazalendo na CHADEMA