
Aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Tundu Lissu
Akizungumza katika mkutano wake kwa njia ya mtandao Lissu, amewashukuru wananchi wote waliojitokeza katika kampeni za chama chake huku akisema kuwa wananchi ndio waliokuwa nguzo katika kipindi chote cha kampeni.
“Tunachotakiwa kufanya ni kufanya kazi kwa bidii na kuwa wavumilivu na licha hayo lazima tuhakikishe muungano na ushirika wetu unalindwa ili kufanya hivyo lazima tuhakikishe muungano wa chama na uongozi wake unazingatiwa, lazima tuendelee kukijenga upya na kukiimarisha chama chetu kupitia CHADEMA ni Msingi, ambayo imetusaidia sana ndani ya miaka mitano, demokrasia lazima Iimarishwe.” amesema Tundu Lissu
Aidha Lissu, amewasisitizia wananchi kuwa huu si muda wa wananchi kukata tamaa huku akiwapongeza viongozi wa vyama, waliokuwa wagombea mbalimbali katika kampeni pamoja na timu nzima za kampeni kwa kupambana na changamoto zilizokuwa zikijitokeza na kufanikisha mchakato mzima wa kampeni.