Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Lugola atembelea njia za Magufuli

Jumatatu , 16th Jul , 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola ametoa siku zisizozidi kumi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho NIDA, akiwa na kampuni ya Iris Dilham kufika ofisini kwake mjini Dodoma ili kueleza sababu ya kutofika kwa mtambo wa kuchapisha vitambulisho mpaka sasa.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola

Agizo la Mh. Lugola linakuwa ni utekelezaji wa miongozo aliyopatiwa na Rais Magufuli siku alipomuapisha kuwa Waziri wa Mambo ya ndani baada ya kutengua uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba.

Wakati akitoa muongozo wa maeneo sugu ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Julai 2 Rais Magufuli alisema "Kuna suala la NIDA, mambo ni hovyo. Kuna pesa zilichezewa, kuna vifaa viliagizwa na havikufika. Tumewachukulia hatua lakini waliofanya mambo hayo mpaka leo hatua gani wamechukuliwa? Je, pesa hizo zimerudishwa? Kasimamie hayo mambo," Rais Magufuli.

Mhe. Lugola amesema hayo baada ya kutembelea Ofisi ya Uzalishaji vitambulisho hivyo kilichopo Kibaha, mkoani Pwani na kutoridhishwa na kazi ya utoaji wa vitambulisho kwa wananchi, zoezi ambalo linaendelea kufanywa na NIDA katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri huyo amesema kuwa mpaka sasa kuna dalili za kuwa kampuni hiyo iliyopewa tenda imeshindwa kuleta mtambo huo hivyo atahitaji maelezo ya kina kuhusiana na hilo kabla hajachukua maamuzi mengine.

"Dalili zinaonyesha kwamba kampuni ya Iris Dilham haina mpango wa kutuletea huo mtambo. Sasa kama hawana mpango ni vyema wakatueleza fedha zetu ziko wapi. Nakuagiza Mkurugenzi Mkuu nataka nikiwa Dodoma Julai 25 mwaka huu majira ya saa nne mfike ofisini kwangu ukiwa na hao wenye kampuni ya Iris, na kwa kuwa wameonyesha kushindwa waje na hizo pesa in 'advance' kabisa ili kusudi tukazihifadhi benki tena tutapeleka na 'escort' ya juu. Ztafanyiwa shughuli nyingine. Hatuwezi kucheza na pesa za watanzania " amesema Waziri Lugola.

Msikilize hapa chini Mh. lugola akitoa maagizo.

HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini

Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari