Jumatano , 22nd Mei , 2024

Mahakama ya wilaya ya Wanging'ombe Mkoa wa Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 Elias Thomas Mwanzalila (30) mkazi wa kijiji cha Igima kwa kosa la kumbaka bibi kizee mwenye umri wa miaka 81.

Elias anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 19, 2024 huko Wanging'ombe mkoa wa Njombe, ambapo katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Jaji Jamsi Emmanuel Mhone Mahakama imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na kumkuta na hatia. 

Hata hivyo, Mahakama imetoa hukumu ya miaka 30 jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo vya ukatili.