Jumanne , 3rd Jan , 2023

Waziri wa Ardhi Angelina Mabula amesema, serikali inakwenda kuchukua hatua za kisheria kwa wamiliki wa vituo vya mafuta ambao walivijenga mara baada ya kanuni kuanza kutumika mwaka 2018 huku akieleza kwamba wale ambao walijenga kabla ya kanuni hizo kuwekwa wao hawatachukuliwa hatua.

Waziri wa Ardhi Angelina Mabula

Waziri wa Ardhi Angelina Mabula, amesema wamebaini kuwepo kwa vituo vingi vya mafuta ambavyo vimejengwa ndani ya hifadhi ya barabara huku wamiliki wa vituo hivyo wakiviendeleza  na wengine wakiendelea kuvijenga licha ya zuio la serikali la hivi karibuni la kusitisha utoaji wa vibali vya ujenzi wa vituo hivyo.

Kuhusu migogoro ya ardhi hapa nchini Waziri ameeleza kupungua na iliyopo kwa sasa ni Ile ya kuanzia miaka ya 1985 mpaka 1990 lakini baada ya mwaka 2015 wanatatua ile ya zamani na kutoruhusu migogoro mipya ya ardhi

Aidha amesema wale ambao wamepewa ardhi na serikali na kutoiendeleza bado wanaendelea kuchukua hatua ikiwemo kunyang'anywa.