Jumapili , 7th Jun , 2020

Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo amesema umefika wakati sasa kwa jeshi kama taasisi nyeti nchini, kuwa na miradi yake binafsi ya huduma pamoja na ile ya uzalishaji.

Jenerali Mabeyo ameyasema hayo eneo la msata wilayani bagamoyo mkoani Pwani wakati wa uzinduzi wa miradi mbalimbali ya huduma na uzalishaji katika shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS kihangaiko.

Amesema hatua hiyo itaokoa matumizi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya kulipia huduma hizo katika utendaji wa kila siku ndani ya taasisi hiyo , ambazo wakati mwingine huwa hazitoshelezi barabara.

Aidha Mabeyo ametolea mfano wa moja ya mradi wa maji aliouzindua, kuwa utasaidia kupunguza matumizi ya fedha ambazo jeshi limekuwa likilipa kwa ajili ya huduma hiyo.

Akitoa maelezo mafupi ya mradi huo Mkuu wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS kihangaiko Kanali Sijaona Myala pamoja na msimamizi wa mradi huo Sajenti Abeid Wilson kwa pamoja wamesema, kulikuwa na kila sababu za kuwa na mradi huo shuleni hapo kutokana na idadi kubwa ya askari waliopo.

Miradi mingine iliyo zinduliwa ni pamoja na Nyumba ya mapumziko ya Viongozi wakuu, Lori la mchanga, jengo la ukumbi wa sherehe na Kisima cha maji.

Tazama video hapo chini