Jumapili , 31st Oct , 2021

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amesema Jumatatu Novemba 1 hadi Jumatano Novemba 3, ndio siku maalum kwa machinga jijini humo kuhamia kwenye maeneo yaliyopangwa kwaajili yao.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella

Aidha Mongella amesisitiza kuwa zoezi hilo sio la kisiasa bali linahusu maisha ya watu na wana mchango kwenye maendeleo ya taifa.