Jumapili , 30th Jan , 2022

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Wizara hiyo itawapima utendaji wao wa kila siku Waganga Wakuu na Waganga Wafawidhi nchi nzima wa vituo vya serikali kwa mambo Sita kulingana na utendaji wao wa kila siku.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Ummy aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga, ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea eneo la kuhifadhiwa dawa kwenye kituo hicho ambapo atawapima watoa huduma zao kuanzia Hospitali za Taifa, Rufaa,Mikoa,wilaya, Zahanati na Vituo vya Afya.

Waziri Ummy ameyataja mambo hayo kuwa ni mapokezi ya mgonjwa na lugha, hiyo ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakipatiwa na wataalamu wa afya pindi wanapofika kupata matibabu. 

Jambo la pili amesema watawapima katika wagonjwa 100 waliofika ni wangapi waliochukuliwa rekodi yao, jambo la tatu watakaloangalia ni historia ya mgonjwa kama amefanyiwa uchunguzi wa kutosha kulingana na tatizo alilonalo. 

Jambo la nne ni watakaliangalia ni mgonjwa kama amepatiwa vipimo vyote anavyotakiwa kupatiwa , jambo la tano ni kuangalia kama mgonjwa amepatiwa dawa anayostahili kupata katika hospitali huku jambo la sita watakaloangalia ni kwamba mgonjwa ametumia muda gani kupata huduma. 

Waziri Ummy amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikishawatanzania wanapata huduma bora za afya na si bora tu huduma kwa kuangalia maeneo hayo 6.

Wakati huo huo Waziri Ummy amepiga marufuku hospitali zote  nchi nzima kuacha kuwatoza fedha kina mama wajawazito nchi nzima na badala yake huduma zote zinazopatikana wapatiwe bure ikiwa ni pamojana huduma ya Ultra sound pamoja na watoto wachanga zitolewe bure ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga.