Jumatano , 23rd Dec , 2015

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi juu ya malalamiko yaliyopo kwa wagonjwa kukosa matibabu hata yale waliyotakiwa kupatiwa bila malipo yoyote.

Waziri Mwalimu ametoa uamzi huo hii leo baada ya kupokea malalamiko ya kuwepo kwa mgongano wa kimaslahi mengi kutoka kwa wagonjwa kuwa upatikanaji wa dawa katika hospitali hiyo si wa kuridhisha hasa zile wanazotakiwa kuzipata bure.

Aidha. Mhe. Mwalimu amewataka watendaji wa sekta ya afya nchini kukiri kwa maandishi endapo wanamiliki Hospitali, maduka ya dawa ama zahanati ndani ya siku 21 kuanzia leo lengo likiwa ni kuziba mianya ya upotevu wa dawa katika hospitali za serikali.