Madiwani watimua wezi wa milioni 118

Jumatatu , 13th Mei , 2019

Balaza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mjini mkoani Ruvuma, limewakuta watendaji wake watatu na hatia ya upotevu wa fedha za manispaa kiasi cha shilingi milioni mia moja na kumi na nane.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mjini, Abdul Hassan Mshaweji

Akisoma maamuzi yaliyofikiwa na balaza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mjini, Abdul Hassan Mshaweji, amesema watuhumiwa walikua wanne na mmoja hajakutwa na hatia.

Pia mwenyekiti huyo wa halmashauri ametaja hatua zilizochukuliwa na Baraza la Madiwani la hamshauri hiyo kwa watendaji watatu waliokutwa na hatia ya upotevu wa fedha, huku kamati ya uchunguzi ikimwachia huru mtuhumiwa mmoja kutokana na kutokutwa na hatia.

"Watendaji wetu watatu wamekutwa na hatia, Juliana Lotti amekutwa na hatia 8 na Baraza la Madiwani kwa masikitiko makubwa limefanya maamuzi magumu na maamuzi ya baraza ni kwamba tumeamua afukuzwe kazi moja kwa moja, wa pili anayefuatia ni Salum Mwandu ambaye baraza limeamua kuzuia mshahara wake nusu kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hali kadhalika mtunza hazina Denis Mwatete, baraza limeamua kuzuia mshahara kwa muda wa mwaka mmoja".

"Mchakato unaendelea na kwa mujibu wa sheria, mamlaka ya mwisho sasa ni kwa Baraza la Madiwani la manispaa. Wahusika katika suala hilo walikuwa wanne, ambapo mmoja ameachiwa huru na kamati iliyofanya uchunguzi, huyu ni mkaguzi wetu wa ndani".

Bonyeza hapa kutazama zaidi.