
Katika kusimamia mkakati wa kuzuia vitendo vya kihalifu limetaja baadhi ya matukio yaliyojiri mwezi uliopita likiwemo lile la tarehe 11 Agosti, 2025 ambapo alikamatwa mtuhumiwa Ramadhan Makala Mkazi wa Tabata kwa tuhuma za kusafirisha bhangi gunia 13 zenye uzito unaokadiriwa kuwa kilogramu 239 kutoka Morogoro kuja Dar es salaam na kuongeza kuwa mtuhumiwa na wahusika wengine watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Katia hatua nyingine, tarehe 12 hadi 20 Agosti, 2025 katika eneo la Magomeni Kinondoni jeshi la polisi liliwakamata watuhumiwa wawili, Hassan Hamis Mkazi wa Tandale na Elia Mapunda Mkazi wa Goba Njia nne wakiwa na pikipiki 6 za wizi pamoja na watuhumiwa watatu waliokuwa wakijihusisha na makosa ya uvunjaji, Gift Shabani Mkazi wa Kimara, Hussein Ally Mkazi wa Tandale pamoja na Razaki Ramadhani Mkazi wa Manzese aliyekutwa na simu 10 za aina mbalimbali ambazo ni za wizi.
Aidha, katika msako wa tarehe 16 hadi 25 Agosti, 2025 yalikamatwa magari 15 yenye namba za usajili usio rasmi wa ‘SSH 2530’ ikiwa ni kinyume cha sheria.
Kuhusiana na matukio ya ukatili kwa binadamu, mwezi Julai hadi Agosti, 2025 Ashiri Bashiru Selemani Mkazi wa Kivule alihukumiwa na Mahakama ya Kinyerezi Ilala kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubakahuku Jumanne Onesmo Ngalya Mkazi wa Chanika akihukumiwa na Mahakama ya Wilaya Ilala Miaka 30 jela kwa kosa la Kubaka, sanjari na Tyson Fidel Malingumu Mkazi wa Yongwe Chanika aliyehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kifungo cha Miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Wengine ni Nicolaus Gabriel Thomas wa Tabata Barakuda aliyehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kifungo cha maisha jela kwa kosa la Kubaka na kulawiti. Shafii Abdallah Shado Mkazi wa Karakata alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kifungo cha maisha Jela kwa kosa la kulawiti . pia, Samwel Kedymo, Mkazi wa Kibamba kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ubungo alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la Unyang’anyi wa kutumia silaha,na Maulid Rashid Mfuko Mkazi wa Mbezi alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo kifungo cha Miaka 30 jela kwa kosa la Unyang’anyi wa kutumia silaha
Kuelekea sikukuu ya Maulid Septemba 5, 2025 Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limetoa wito kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu kwa watoto wakati wa matembezi na mikusanyiko mbalimbali ili kusherehekea Sikukuu hiyo kwa amani na utulivu huku suala la usalama barabarani likisisitizwa kwa madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara ili kuepusha ajali.