
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Magonjwa yasiyo ambukiza Tanzania, Dkt. Andrew Swai amesema, ili kuepukana na magonjwa ya aina hiyo Serikali kupitia wataalam mbalimbali wa afya wanawajibu wa kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa umma juu ya athari na namna ya kukabiliana na magonjwa hayo.
Amesema magonjwa hayo yanasababishwa na mtindo wa maisha hasa kutokufanya mazoezi ya mwili pamoja na kutumia vitu vyenye sukari na chumvi nyingi.
Dkt. Swai amesema kati ya magonjwa hayo, ugonjwa wa 'presha' unaonekana kuongoza kwa vifo kwani ugonjwa huo husababisha vifo kwa asilimia 27 kutokana na kutokuwa na dalili na mara nyingine watu kuhisi kuwa wamerogwa.
Chama cha Madaktari wa Magonjwa yasiyo ambukiza Tanzania kimetoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanaripoti na kuandika taarifa za magojnwa hayo kwani ndio yanaogoza kwa kusababisha vifo.