
Dkt John Magufuli - Mwenyekiti CCM Taifa
Akiongea leo katika mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine kikao hicho kimefanya mabadiliko ya kimuundo na kiutawala, Dkt. Magufuli amesema anataka kuona chama kinakuwa mali ya wanachama badala ya chama kuwa ,chama mali ya mwanachama.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ametangaza mabadiliko hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo amesema NEC imepunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya maamuzi ya chama pamoja na idadi ya vikao vya chama kutoka wajumbe 388 hadi kufikia 158.
Amesema kwa upande wa vikao vya halmashauri kuu ya taifa kufanyika baada ya miezi sita badala ya miezi miinne ya awali pamoja na NEC kukutana mara mbili badala ya mara tatu ikiwemo kupunguza idadi ya wajumbe kutoka 34 hadi 24.
Ameongeza kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na halmashauri kuu imewateuwa wajumbe wapya ambao watachukua nafasi zilizoachwa wazi baada ya wajumbe waliokuwepo kuteuliwa katika nafasi mbalimbali za kiserikali ambapo amesema wamemteua Humphrey Polepole kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM.
Wengine ni pamoja na Rodrick Mpogolo ambaye amekuwa naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara na Kanali Ngemela Lubinga kuwa katibu wa halmashauri anayeshughulikia siasa na uhusiano wa kimataifa.