Jumapili , 1st Nov , 2020

Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, leo Novemba 1, 2020, amekabidhiwa cheti cha ushindi wa nafasi hiyo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Semistocles Kaijage.

Magufuli akipokea cheti cha ushidni kutoka kwa Jaji Semistocles Kaijage

Hafla hiyo ya kukabidhiwa cheti cha ushindi, imefanyika jijini Dodoma ambapo kabla ya kukabidhi, Jaji Kaijage alisema uchaguzi ulienda vizuri kuanzia Oktoba 28 zoezi la upigaji kura lilipoanza, hadi Oktoba 30, alipotangazwa mshindi wa urais.

Aidha Jaji Kaijage pia amemkabidhi cheti cha ushidni Makamu wa Rais mteule ambaye ni Samia Suluhu Hassan.

Mama Samia Suluhu akipokea cheti cha ushindi wa nafasi ya Makamu wa Rais

Baada ya kukabidhiwa cheti hicho, Magufuli ameishukuru tume kwa kuendesha uchaguzi wa huru na haki pamoja na kufanikisha kukamilika kwa zoezi hilo mapema.

Bonyeza hapo chini kutazama shughuli nzima