
Bi. Riziki Said Lulida
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo na Mkurungezi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, imeeleza kuwa uteuzi huo umefanyika leo Novemba 29, 2020.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Bi. Riziki, ataapishwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bi. Riziki amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo, kuwa Mbunge wa Viti Maalum (CUF) mkoa wa Lindi.
Bi. Riziki Said Lulida enzi akiwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi
Pia Bi. Riziki amewahi kuwa Mwenyekiti wa kusimamia Mazingira,Urithi wa Dunia na Wanyamapori ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.