
Humphrey Polepole
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa leo na Mkurungezi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, imeeleza kuwa uteuzi huo umefanyika leo Novemba 29, 2020.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Polepole ataapishwa kwa mujibu wa Sheria na taratibu za bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbali na kuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Polepole ameshawahi kuwa Mkuu wa Wilaya katika wilaya za Musoma na Ubungo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inampa mamlaka Rais kuteua wabunge 10 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.