Magufuli awashangaa Wazaramo Jokate kutokuolewa

Jumapili , 28th Jun , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amewashangaa watani zake Wazaramo kwa kushindwa kumuoa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ili hali hana Mume.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Juni 28, 2020, alipokuwa akiwahutubiwa wananchi wa Kisarawe mara baada ya kuzinfua mradi wa maji wa Kibamba hadi Kisarawe uliogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 10.6.

"Hata mkuu wa Wilaya wa hapa amefanya kazi nzuri katika kuondoa Zero , hapa kulikuwa na Zero nyingi sana, ninachowashangaa watani zangu Wazaramo hajaolewa, lakini mmeshindwa kumuoa mnamuangalia tu, ndiyo shida ya wazaramo saa zingine mnashindwa mambo" amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amempongeza Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo kwa utendaji wake wa kazi, "Nimpongeze Jafo kwa kunisaidia kazi, kijana huyu anajituma sana, mwembamba kwa umbo lakini mambo yake makubwa anazunguka kila mahali, sijasema Mawaziri wengine hawafanyi kazi lakini nipo kwenye jimbo la Kisarawe".