Magufuli awaonya aliowateua

Jumanne , 29th Jan , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kutotumia mamlaka yao vibaya kwa kuwaweka ndani baadhi ya watendaji wenzao ikiwa ni kinyume na sheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya 2 Mwanga pamoja na Tarime ambapo alibainisha sababu za kuwatengua waliokuwa kwenye nafasi hizo kuwa ni kutokana na kutumia vibaya mamlaka yao.

Rais Magufuli amesema, "mnasheria na mamlaka mlizopewa msizitumie vibaya sheria mnazo lakini msizitumie vibaya mtu anawekwa ndani halafu hamumpeleki mahakamani".

"Viongozi wengi wamelizungumzia hili namimi nalirudia, kuna masuala mengine hayahitaji mtu kuweka ndani yanahitaji kutoa maelekezo tu"

Aidha Rais Magufuli amehoji juu ya hatua mtu anayetuhumiwa kubaka watoto 11 kushindwa kukutwa na hatia na mahakama baada ya ushahidi kutojitosheleza.