Magufuli,Kikwete wakwama, sherehe ya Mapinduzi

Jumamosi , 12th Jan , 2019

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Alli Mohamed Shein ametaja sababu za kutokuwepo kwa baadhi ya viongozi kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Mstaafu Kikwetena Rais wa sasa Dkt John Magufuli

Akizungumza kwenye hadhara hiyo Rais Shein amesema sababu iliyowafanya Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli, kuwa ni viongozi kupatwa na dharula.

Akizungumzia miaka 55 ya mapinduzi Rais Shein amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itaendelea kulinda usalama wa nchi na kudumisha upendo na amani.

Ninawahakikishia kuwa nchi yetu iko salama na itaendelea kubaki salama na serikali zetu mbili zitaendelea kutimiza majuku yake ipasavyo na tutahakikisha amani na utulivu vinadumishwa na sheria zote zinafuatwa."

Mimi na rais Magufuli tutahakikisha Muungano wetu unadumu kwa dhamira ile ile ya viongozi wetu waliopita ili nchi yetu izidi kubaki na amani”, amesema Dkt Shein.