Alhamisi , 6th Aug , 2020

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata amesema kuwa Mahakama nchini hazijapokwa mamlaka ya kusikilza maombi ya dhamana kwa makosa ambayo yanaruhusu kutolewa dhamana.

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata akisisitiza jambo wakati akizungumza na wa habari leo.

Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata amesema kuwa Mahakama nchini hazijapokwa mamlaka ya kusikilza maombi ya dhamana kwa makosa ambayo yanaruhusu kutolewa dhamana.

Amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua pia haki ya jamii kulindwa dhidi ya madhara yanayoweza kutokana na baadhi ya vitendo vinavyohusisha makosa ya jinai kama vile mauaji, utakajishaji fedha, ugaidi na usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza na vyombo vya habari Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata amesema kuwa kesi iliyofunguliwa na Bwana Dickson Sanga dhidi ya serikali ilishindwa kihalali kwani lazima jamii pia ilindwe ili kulinda Afya, Ustawi wa Jamii na kukuza uchumi.

Jana Agosti 5, 2020 Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilitoa uamuzi wa Rufaa Na. 175/2020 iliyokatwa na serikali dhidi ya Dickson Paul Sanga kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu mwenendo wa mashauri ya jinai kinachozuia dhamana kwa baadhi ya makosa makubwa ya jinai.