Ofisi za makao makuu ya NCAA
Amefanya maamuzi hayo leo alipotembelea Ofisi za makao makuu ya NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.
"Haiwezekani mtumishi awe anachunguzwa na TAKUKURU halafu aendelee kuwa ofisini si atavuruga uchunguzi. Asimamishwe kazi kuanzia leo mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika na aikibainika kwamba hana hatia atarudi kazini,” alisema.
Pia Waziri Mkuu alimtaka Mkurugenzi Mkuu wa NCAA, Fred Manongi kueleza zilipo sh. bilioni moja zilizotolewa na Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete kwa ajili ya kujengea ranchi ya wafugaji wa tarafa ya Ngorongoro.
Akijibu swali hilo Manongi alisema wakati Rais Kikwete anatoa fedha hizo alikuwa bado hajateuliwa kushika washifa huo, ambapo Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi huyo kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo na kasha kumpelekea tarifa.