Jumatano , 20th Jul , 2016

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuzindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Dodoma, ili uweze kupokea ndege kubwa za mizigo,abiria na viongozi wa kitaifa na kimataifa.

Uwanja wa Ndege Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amesema leo waziri Mkuu atazindua ukarabati wa uwanja huo kwa Niaba ya Rais Magufuli na kuongeza kuwa uzinduzi huo hakutaathiri ujenzi wa uwanja wa Kimataifa eneo la Msalato.

Ujenzi na ukarabati wa uwanja huo unatarajiwa kuhgarimu shilingi bilioni 11.5 ambazo ni fedha za ndani na utatoa fursa kwa mashirika ya ndege kuanza huduma Dodoma ikiwemo ndege ambazo zitanunuliwa na serikali.

Rugimbana amesema kwa sababu kubwa ya kupanuliwa kwa uwanja huo ni nia ya dhati ya rais Magufuli ya serikali yake kuhamia Dodoma na kusema mara baada ya awamu hiyo ya kwanza awamu ya pili itafanyika haraka ili kukamilisha mpango huo.