
Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 5, 2022, majira ya saa 2:00 usiku katika Kijiji cha Kisongo Pande wilayani kilwa mkoani humo.
"Watu hawa walikuwa wanne, wawili waliingia ndani na wawili walibaki nje na kupiga risasi juu ili kuwatisha wananchi na yule aliyevamiwa walioingia ndani walipora milioni 1.2, kutokana na Polisi Kata na ulinzi shirikishi wananchi waliweza kujikusanya na kuwadhibiti majambzai hao,"amesema Kamanda Kitinkwi