Jumatano , 18th Dec , 2019

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Hamis Musa, amesema kuwa wakati wanatoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo, hawakuwa na nia mbaya ya kuvuruga amani ya nchi, bali ni yao ni kutetea haki ya wanafunzi ambao wana uhitaji.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Hamis Musa.

Akizungumza leo Disemba 18, 2019 na EATV & EA Radio Digital, Rais huyo wa DARUSO amesema kuwa hadhani kama agizo la Waziri wa Elimu la kutoa masaa 24 kwa uongozi wa chuo ili wao waweze kuchukuliwa hatua kama lilikuwa ni sahihi.

"Lakini sisi lengo letu sio baya, wala hatuna lengo la kuharibu amani ya nchi hii sisi tuna lengo la kutetea haki za wanafunzi, kwahiyo Waziri alivyosema vile sidhani kama alikuwa sahihi sana, sisi tunawakilisha wanafunzi na hawajui shida wanazokutana nazo" amesema Rais wa DARUSO.

Hata hivyo tayari Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, umekwishatekeleza agizo la Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako, na tayari wamewasimisha baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi akiwemo Rais wao.