Ijumaa , 22nd Oct , 2021

Malkia Elizabeth (95) wa Uingereza ameshauriwa na wataalamu wa Afya kupumzika kwa muda baada ya uchunguzi wa awali kufanyika na matabibu kufuatia kulazwa Hospitali siku ya Jumatano.

Picha ya Malkia Elizabeth

Malkia ameruhusiwa kutoka Hospitali siku ya Alhamisi na kurudi nyumbani kwake Windsor Castle huku taarifa kutoka jumba la kifalme zinasema kuwa matatizo yake ya kiafya hayahusiani na COVID-19.