
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Akihutubia katika Baraza kuu la Umoja wa wanawake, UWT, linalofanyika leo Agosti 10, 2020 Jijini Dodoma, amesema anatumaini viongozi wote waliopita kwenye mchujo hapo awali ni viongozi bora ambao sio wapokeaji wala watoaji rushwa.
''Kiongozi mzuri ni yule ambaye anapata uongozi kwa weledi bila rushwa, anayejiamini sasa mjitathimini mkishindwa kujipanga huku chini huko juu tutawapanga'', amesema Mama Samia.
''Jukumu la kulainisha mchakato limeachwa kwenu UWT, hivyo mnatakiwa kujitoa hasa,jukumu lililopo mbele yenu ni zito na sio jepesi kama mnavyodhania'', ameongeza.
Aidha amesema kuwa Jumuiya za CCM zinatakiwa kujidhatiti ili kupata ushindi kwa pande zote mbili bara na visiwani.