Jumapili , 3rd Jan , 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, amefika General Hospital Dodoma na kuwafariji majeruhi wa ajali ya treni iliyotokea jana Januari 2, 2021 Dodoma. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akiwaona baadhi ya majeruhi

Akiwa hospitalini hapo Mama Samia amesema amtembelea wodi zote na kuwaona majeruhi ambapo wengi wao wanaendelea vizuri.

Aidha ameeleza hatua ambazo zimechukuliwa mpaka sasa ikiwemo kuwasaidia usafiri wa kuendelea na safari abiria waliotoka salama pamoja na majeruhi wanaopona.

Zaidi tazama Video hapo chini