'Man of the Match' azawadiwa AK-47

Jumapili , 15th Sep , 2019

Kipa Saveli Kononov wa timu ya Izhstal Izhevsk(23), nchini Urusi, amepewa zawadi ya silaha aina ya AK-47 baada ya kuibuka mchezaji bora wa mechi, walipocheza dhidi ya Chelmet Chelyabinsk.

Mechi hiyo ilichezwa mapema wiki hii, na timu yake iliibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya wapinzani wao.

Zawadi hiyo alipewa katika vyumba vya kubadilishia nguo kutoka kwa viongozi na nahodha wa timu ambapo wamesema "tunatoa zawadi hii kwa alivyosaidia kupangua mashuti 36 kati ya 38 yaliyolenga goli, ikitokea tumecheza vibaya basi atatushoot nayo"

Katika ligi ya 'The National Hockey League' ni utamaduni uliozoeleka wa kutoa zawadi zisizo za kawaida kwa wachezaji watakaocheza vizuri.

Zawadi nyingine iliyotolewa ambayo ilishangaza ni mchezaji wa timu ya Carolina Hurricanes, baada ya kutangazwa kuwa 'Man Of The Match' alipewa zawadi ya shoka.