
Mfano wa magunia yenye takataka
Akizungumza na Kurasa hii leo Mjumbe wa mtaa huo, Abdallah Juma, amesema kumekuwepo na mgogoro wa uzoaji taka baina ya wafanyabiashara waliopo eneo hilo wakidai kuwa fedha wanayolipia kwa ajili kitambulisho cha mjasiriamali kinajumuisha tozo hiyo.
Amesema adha hiyo imesabisha kutoelewana kati yao na wakandarasi sababu ya kushindwa kuwalipa fedha kwa ajili ya kuleta magari ya kubebea taka hizo
Naye Mwenyekiti wa mtaa huo, Nestory Kobelo, amesema kuwa inawalazimu kuondoa taka hizo wenyewe pindi zinapotolewa ili kuepusha uchafuzi wa mazingira.