Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Dkt. Abdallah Possi,
Akizungumza leo Bungeni mjini Dodoma, katika Kipindi cha Maswali na Majibu, Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Ulemavu), Dkt. Abdallah Possi, amesema kuwa serikali inaendelea kufanya jitihada za kupambana na biashara hiyo na mpaka sasa wafanyabiashara wakubwa kadhaa wanashikiliwa na kesi zao zinaendelea.
Aidha Dkt. Possi ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano imeamua kuimarisha uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla ili kuondoa ugumu wa maisha ambao ndio unasemekana ndio chanzo cha vijana wengi kujiingiza katika utumiaji wa dawa hizo.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa serikali inapata ugumu wa kupambana na biashara hiyi kutokana na kufanywa kwa kificho huku pia watumiaji wengine wa dawa hizo ni watu wenye uwezo wa kimaisha sio masikini kama dhana ilivyojengeka nchini.
Dkt. Possi amewataja baadhi ya wafanyabiashara wakubwa waliokamatwa kwa tuhuma za uuzaji wa dawa za kulevya ni pamoja na Ally Khatibu Khaji maarufu kwa jina la Shkuba,Mohammed Muharami Maarufu kwa jina la Chonji na Mwanaidi Mfundo maarufu kwa jina la Mama Leyla.
Aidha Dkt. Possi ameongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali wanatoa huduma za upataji nafuu katika vituo mbalimbali lakini ipo katika mchakato wa kujenga kituo kikubwa Mkoani Dodoma na Tanga kwa ajili ya kutoa hduma kwa waathirika wa dawa hizo.