Marin Hassan wakati wa uhai wake
Marin Hassan Marin amefariki Dunia asubuhi ya leo April 1, 2020, katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
Katika salamu zake za rambirambi kwa uongozi wa TBC na wafanyakazi kiujumla, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameonesha kuguswa na msiba huo na kueleza kuwa alikuwa mwandishi aliyeripoti taarifa zake kwa ubunifu na mvuto wa hali ya juu.
Aidha Rais Dkt Magufuli amejitolea ndege yake binafsi, ambayo imechukua ndugu wa marehemu walioko mkoani Dodoma, na kuletwa Dar es Salaam.