Niger imekua ikikumbwa na mafuriko kila mwaka lakini mafuriko ya mvua za msimu wa mwaka huu yameua watu mara mbili zaidi ya mwaka jana .Mafuriko hayo pia yameua mamia ya mifugo na pia kuharibu mali ikiwemo mashamba makubwa ya chakula.
Waziri anayehusika na ,masuala ya kibinadamu nchini humo Bw. Lawan Magaji, amesema kwamba katika mikoa ya Maradi, Zinder na Diffa iliathiriwa vibaya na mafuriko hayo.
Karibia watu 150,000 walilazimika kuyahama makazi yao kwenye mikoa hiyo mitatu.
Nchi kadhaa zilizopo Afrika Magharibi zikiwemo Nigeria,zimekua zikikumbwa na mafuriko makubwa na mvua kali huku wataalamu wakisema kwamba sababu kubwa ni mabdiliko ya hali ya hewa.

