Ijumaa , 6th Dec , 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, amepiga marufuku viongozi wa Serikali kuzuia barua za watumishi kufika eneo linalohusika na kwamba hata kama inakwenda kwake ni lazima iachwe na imfikie.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo leo Desemba 6, 2019, Jijini Dodoma, ikiwa ni kuelekea kwa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu, ambapo amesema baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa ni chanzo cha uvunjifu wa haki za binadamu hivyo lazima wabadilike vichwani mwao.

Aidha Mkuchika amewaonya viongozi wanaowafukuza kazi watu ambao hawajawateuwa na hawana mamlaka nao kwani kwakufanya hivyo ni ukiukaji wa Haki za Binadamu.