Alhamisi , 5th Mei , 2016

Chama cha Forum for Democratic Change kilitangaza hivi karibuni kwamba kitaanzisha maadamano ya kupinga ushindi wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuapishwa kwake Mei 12 2016.

Kufuatia tangazo hilo serikali ya nchi hiyo imepiga marufuku ya kufanya maandamano au kupinga ushindi wa mwezi Februari wa Rais Museveni hadharani.

Kiongozi wa kambi ya upinzani ambaye alitarajiwa kuongoza maandamano amewekewa kizuizi tena nyumbani kwake na haruhusiwi kutoka nje.

Aidha Mji wa Kampala umezingirwa na wanajeshi huku vyombo vya habari vikiarifiwa kutokufanya matangazo ya moja kwa moja kuhusiana na kupingwa kwa ushindi wa Rais Museveni.