Jumanne , 20th Sep , 2016

Kampuni ya simu za mkononi Vodacom kwa kushirikiana kampuni ya vinywaji baridi ya Coca- Cola wanatarajia kutoa zawadi lukuki kwa mashabiki watakaofika kushuhudia fainali za Dance100% 2016 zinazofanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Don Bosco, DSM

Kundi la J Combat

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo linaloendeshwa na EATV, Bhoke Egna amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kutazama fainali za shindano hilo ambapo makundi 6 yatapambana ili kuweza kupatikana mshindii mmoja atakayeibuka kidedea.

“Shindano la fainali itafana sana kwa sababu kampuni zote tutatoa zawadi kwa mashabiki kwa maana ya Vodacom, Coca- Cola pamoja na EATV ambapo pia kuna watu watapatiwa tiketi za kutazama EATV Awards hivyo watu wasikose shindano hili.

Aidha makundi yote sita ambayo yatapambana hatua ya fainali yanaendelea na mafunzo chini ya majaji wa dhindano hilo ambapo majaji wamegawana makundi ili kufanikisha shughuli hiyo.

Shindano la Dance100% linaoneshwa na kituo cha EATV pekee kila Jumapili saa moja jioni na matukio yote ya shindano yataoneshwa.

Tags: