Ijumaa , 23rd Feb , 2018

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amekanusha habari zinazosambaa kwa kasi kati mitandao ya kijamii kuhusu yeye kusafirisha watu kwenda kuzuuru nchi ya Israel na kusema hao ni matapeli na wanapaswa kupuuzwa.

Mh. Nyalandu amekanusha taarifa hiyo kupitia mitandao yake ya Facebook na Twitter na kusema kwamba anasikitishwa na watu hao ambao wanakaa na kuwatungia wenzao uongo.

Fake News alert❗Habari hii ya kupeleka watu Israel sio ya kweli na Account iliyotumika kuandika sio yangu. Tafadhali ipuuzeni. So many sad people out there wanaokaa kutungia wenzao UONGO. Sad!,”ameandika kwenye kurasa zake za mitandao yake  kijamii kuutarifu umma na kuweka tangazo hilo.

Taarifa  hiyo ambayo Facebook iliyoandikwa na mtu anayejiita Lazaro Nyalandu inasema kwamba, "Shalom wapendwa kwa wale anaopenda kwenda kutembelea nchi ya Israel ningependa kuwataarifu kwamba wafadhili wamekubali na kulipa gharama zote. Akitokea mtu amekuomba hata hela ya fomu ni tapeli huyo nijulishe haraka. Upendeleo ni kwa Watanzania".

Mpaka sasa inadaiwa kwamba watu zaidi ya400 wameshaomba kwenda kuzuru nchini Israeli baada ya tangazo hilo kuwekwa na mtu huyo anayejiita Lazaro Nyalandu.