Ijumaa , 25th Jan , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amebainisha kuwa mpaka kufikia mwaka 2020 atahakikisha kuwa katika wilaya yake ya wamepania mpaka kufikia mwaka 2020, wanafunzi waliopata sifuri watakuwa wamepungua kutoka kwenye matokeo ya sasa.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo

Kwa mujibu Mwegelo kwa mwaka 2018 kwenye matokeo ya kidato cha nne wilaya hiyo imepata jumla ya ufaulu 175, huku ikiwa imepungua ukilinganisha na miaka nyuma iliyopita.

Jokate ameandika, "niwapongeze walimu, wazazi, walezi na uongozi mzima wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe kwa kuongeza ufaulu wa kidato cha nne 2018 kutoka asilimia 70 mpaka asilimia 82.81".

Aidha Jokate amesema kuwa, "kwa mwaka 2016 ufaulu wa sifuri ulikuwa 457, mwaka 2017 sifuri zilikuwa 259 na matokeo yaliyotoka jana 2018 sifuri zilikuwa 175, na tunatarajia mpaka 2020 tutatokomeza sifuri zote".

Mapema mwaka jana Mkuu huyo wa Wilaya alitambulisha kampeni ya Tokomeza Zero ili kukabiliana na tatizo la ufaulu hafifu wilayani kwake.