Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mauaji ya watoto Njombe, Askofu ataja 'wahusika'

Jumatatu , 4th Feb , 2019

Wakati watoto saba wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wakiripotiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani Njombe, Askofu wa Kanisa la Ufunuo Tanzania Mkoa wa Geita, Heryyabwana Majebere, amesema mauaji hayo yamezuka hivi sasa ikiwa ni kuelekea kwenye

Moja ya mwili wa mtoto ambaye alikuwa ameuawa mkoani Njombe mapema wiki iliyopita

uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kwa mujibu wa Askofu Heryyabwana Majebere, huenda wahusika wakubwa wa mauaji ya watoto ni viongozi wa serikali na vyama vya siasa ambao ndiyo wateja wakubwa wa waganga wa jadi.

Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo katika ibada maalumu ya kuwaombea watoto hao wasio na hatia, Askofu Majebere amesema amepokea kwa masikitiko mauaji ya watoto yanayoendelea Mkoani Njombe huku akibainisha kuwa watoto wana haki ya msingi ya kulindwa.

kuhusu mauaji hayo kuhusishwa na imani za kishirikina, Askofu Majebere amesema serikali inapaswa kuchukua hatua kali kwa waganga watakaobainika kujihusisha na ramli.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kupitia Kamanda wa Mkoa Renata Mzinga limesema linawashikilia watu 28 wakiwemo wafanyabiashara kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watoto ambayo yameonekana kushika kasi hivi karibuni.

HABARI ZAIDI

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa