
Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. Anjela Kairuki
Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. Anjela Kairuki ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Dimani mhe. Hafidhi Ali Tahir ambaye alitaka ufafanuzi mawaziri wakuu wastaafu kujihusisha na siasa wakati huo huo bado wanahudumiwa na serikali na kuitaka sheria hiyo ifanyiwe marekebisho.
Waziri Kairuki amesema kuwa mawaziri wakuu wastafu wana haki ya kujiunga na chama chochote au kujihusisha na masuala ya kisiasa kwakua ni haki yao kikatiba na haki hizo haziwezi kuingiliwa.
Wakati huo huo Waziri Kairuki amekemea tabia ya watumishi wa serikali ambao wanahudumia jamii kwa kubagua matabaka ya vyama, kuwataka waache mara moja na watekeleze sera za serikali kwa kutambua kuwa nchi ina mfumo wa vyama vingi.