Maxence Melo akifikishwa mahakamani leo
Mahakimu waliosikiliza kesi inayomkabili mtuhumiwa Maxence Melo ni Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, Hakimu Mkazi Thomas Simba pamoja na Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa wote wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu.
Akisomewa shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa mtuhumiwa mtuhumiwa Maxence Melo alizuia kuharibu data ambazo Jeshi la Polisi wamekuwa wakizitaka kwa ajili ya uchunguzi kwa kutumia sheria ya uhalifu wa kimitandao.
Shtaka la pili ilidaiwa kuwa kati ya Aprili mosi mwaka huu hadi Desemba 13, katika eneo la Mikocheni Dars es Salaam mtuhumiwa Maxence Melo huku akijua kuwa jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa makosa ya kimtandao kwenye mtandao wake amegoma kutoa ushirikiano wa kutoa data kwa jeshi la polisi.
Maxence Melo
Katika shtaka la tatu ilidaiwa kuwa kati ya Desemba 9 mwaka 2011 mwaka huu hadi Desemba 2016 katika eneo la Mikocheni Dars es Salaam mtuhumiwa Maxence Melo alifanya kosa la kumiliki tovuti ambayo haina kikoa cha Tanzania (dot tz) kinyume na sheria.
Kwa kosa la kwanza hakimu alitoa dhamana ya shilingi milioni 10, kosa la pili dhamana milioni moja na kosa la tatu dhamana milioni 5, ambapo alifanikiwa kupata dhamana ya kosa la kwana za la pili na kukwama kosa la tatu kutokana na mdhamni mmoja kukosa vielelezo kwa wakati na kurudi rumande.
Akiongea nje ya Mahakama mara baada ya kumalizika kusomwa mashtaka hayo matatu Johannes Karungura Mwanasheia Mwandamizi Kuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) alikuwa na haya ya kusema.
Wakili Jebra Kamoble
Kwa upande wake wakili Jebra Kambole ambaye anamtetea Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo Mubyazi aliyekuwa na haya ya kusema.