Jumatatu , 14th Sep , 2015

Ufunguzi wa kampeni za wagombea ubunge umeendelea katika mikoa tofauti na vyama tofauti ambapo jana huko mkoani Iringa na Moshi na jijini Dar es Salaam wagombea ubunge wa majimbo hayo walianza kampeni rasmi.

Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa kampeni

Akihutubia umati wa watu waliojitokeza katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika viwanja vya Mlandege mkoani Iringa mbunge aliyemaliza muda wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Mchungaji Msingwa aliwataka wananchi wa mkoa huko kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya kupiga kura mwezi Oktoba bila kuhofia chochote.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Moshi mjini kupitia Chama cha Mapinduzi Bw, Davis Mosha akiongea na wananchi waliojitokeza kusikiliza sera zake amesema kuwa akiingia madarakani atatumia mshahara wake wote kwa ajili ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Kwa upande wake mgombea Ubunge jimbo la Ubungo Bw. Said Kubenea akifungua kampeni zake jijini Dar es Salaam amewataka wananchi kumchagua ili aweze kwenda kuwafichua mafisadi bungeni kutokana na kazi hiyo ameianza toka akiwa muandishi wa habari.