Jumatano , 29th Jul , 2015

Miradi yenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni 3.63 imezinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi katika wilaya ya kigoma wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulifikishwa mkoani Kigoma jana.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Juma Chum Khatibu na Mkimbiza mwenge mwezake wakiwatwisha ndoo za maji wananchi katika moja ya miradi ilizinduliwa na Mbio hizo.

Moja ya Miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa ufugaji nyuki katika Shule ya sekondari Kidahwe ambapo wanafuzni hao walikabidhiwa Jumla ya mizinga 50 ya asali ili waweze kuiendeleza.

Akisoma risala kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwakilishi wa Wanafunzi hao Toi Msafiri amesema mradi huo umeanzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya ufugaji nyuki kwa wanakijiji na wanafunzi katika shule hiyo kwa lengo la kukuza kipato.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge Juma Khatibu amesema mradi huo wa zinga ya nyuki uliokabidhiwa kwa uwe wa msaada katika masuala kukuza kiwango cha elimu sanjari na kuhakikisha wanapata elimu ya ujasiriamali ya ufugaji na uzalishaji wa Asali.