Alhamisi , 22nd Jul , 2021

Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe anashikiliwa kwa tuhuma za kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwepo kuua viongozi wa serikali ambapo wenzeka sita walishafikishwa Mahakamani.

Kushoto ni Msemaji wa Jeshi la polisi SACP David Misime na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe

Akizungumza na wanahabari Msemaji wa Jeshi la polisi SACP David Misime amesema wamefikia uamuzi huo kutokana na uwepo wa upotoshaji mkubwa juu ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo kuwa ni kwasababu ya kupanga na kuandaa kongamano la katiba mpya mkoani Mwanza.

Amesema, jeshi la polisi halitosita kumfikisha mahakamani endapo watabaini kuna sheria aliyoivunja kutokana na uchunguzi unaoendelea kufanyika mkoani Mwanza juu ya kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.