Jumapili , 8th Dec , 2019

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mboweanatarajiwa kushiriki kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru zinazotarajiwa kufanyika Disemba 9, jijini Mwanza.

Mwenyekiti CHADEMA Freeman Mbowe

Hii inakuwa kwa mara ya kwanza kwa CHADEMA kushiriki Sherehe hizo tangu mwaka 2015, ambapo walikuwa wakieleza sababu mbalimbali za kutoshiriki.

Kwa mujibu taarifa iliyotumwa na uongozi wa chama hichi kutoka kwenye kikao cha Kamati Kuu imesema ujumbe wa Kamati ya chama hicho utawasilishwa na Mwenyekiti wake Mbowe.

Kwa sasa Kamati Kuu ya chama hicho iko jijini Dar es salaam kwa ajili yakupitisha wagombea mbalimbali wa chama hicho, katika uchaguzi wake wa ndani wanaofanya hivi sasa.