Ijumaa , 4th Mar , 2022

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ameachiwa huru.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe

Mbowe pamoja na wenzake watatu wameachiwa huru leo Machi 4, 2022, na Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yanawakabili.

Mbowe na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na ugaidi, ambao walitakiwa kuanza kujitetea hii leo.