Jumamosi , 9th Feb , 2019

Mbunge wa Siha, Dkt. Godwin Mollel (CCM) amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi ulikuwa ni mpango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Dkt. Mollel ameeleza kwamba CHADEMA waliamua kumpiga risasi tundu Lissu kwa kuwa alionekana anatengeneza umaarufu binafsi na wao wanataka kuuza nchi ndipo walipotumwa watu ambao wamemsababishia majeraha sasa hivi.

Akitilia msisitizo kauli yake, Mollel amesema kwamba katika mabomu ya Arusha yeye alikuwa ni Daktari aliyeiwakilisha CHADEMA kwenye Post moterm na alipotoka aliwataarifu viongozi wenzake juu ya sampuli alizoziiba na kutaka zipelekwe nchi ya Afrika Kusini lakini viongozi hao hawakuzifanyia kazi.

“Mimi nilikuwa huko lakini nilikimbia kwa mipango yao" Mollel.

Hata hivyo, wabunge wa Frank Mwakajoka (Tunduma) na Joseph Selasini (Rombo), kwa nyakati tofauti waliomba kutoa taarifa kuhusu hoja ya Mollel ambapo walimtaka mbunge huyo kuthibitisha kauli zake na kutovunja kiapo chake cha udaktari.

Akijibu kuhusu taarifa hiyo, Dkt. Mollel alidai kuwa ili athibitishe anataka (Chama wanachotoka wabunge hao) (CHADEMA) waeleze wanakopeleka ruzuku za chama hicho.

Awali Mollel alikuwa ni mbunge wa CHADEMA na baadaye kuhamia CCM ambako aligombea tena na kurejea bungeni akiwa amebadili chama, ameliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa yeye aliiba sampuli ambazo chama hicho kilimkataza kuzitumia.