Mbunge Ndanda, amtaka Mbowe awapishe wengine

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe, amesema kuwa huu ni wakati wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, kuacha ngazi na kuwapisha watu wengine, ambao anaamini wanayosifa ya kushikilia wadhifa huo kwasasa.

Mwambe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache tu, baada ya Mbunge huyo kuonesha nia ya kutaka kugombea Uenyekiti wa CHADEMA kwa kile alichokidai anaamini  anasifa za kukiongoza chama hicho.

''Tunamshukuru Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, kwa mnchango mkubwa alioutoa kwenye chama chetu ila nadhani sasa umefika wakati wa kuwaachia wengine" amesema Mwambe

Hivi karibuni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, alikiandikia barua chama hicho akikitaka kujieleza kwanini kisichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kufanya uchaguzi wa ngazi ya Kitaifa ili kuchagua uongozi mwingine, baada ya uliopo kwa sasa chini Mwenyekiti Freeman Mbowe kufikia ukomo wake Septemba 14, 2019.