Jumatatu , 10th Aug , 2015

Mbunge wa Viti Maalum CUF kutoka mkoani Mtwara Diana Clara Mwatuka amefariki dunia jioni ya leo kwa ajali ya gari.

Pichani gari aliyopata nayo ajali Mbunge huyo na picha ndogo ni picha ya Mh. Diana Clara Mwatuka

Mamlaka husika bado hazijapatikana kutoa Maelezo lakini mashuda wanasema kuwa ajali hiyo imetokea mkoan Mtwara ambapo Diana alikuwa katika gari yake binafsi.

Naibu Mkurugenzi wa mawasiliano wa CUF Abdul Kambaya amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 katika mteremko wa Ndanda na mume wa marehemu aliyekuwemo kwenye gari hiyo amenusurika lakini hali yake ni mbaya.