Mercy Ship Africa ni moja ya meli kubwa duniani, ambayo inafanya ziara zake nchini Afrika na kutoa huduma mbali mbali za kiafya kwa watu wasio na uwezo wa kupata huduma bora za afaya na matibabu yake.
Ilianzishwa mwaka 1978 na Don Stephen akiwa na mkewe Deyon Stephens lakini ile inayotoa huduma Afrika ilianzishwa mwaka 1999 kwa misaada ya watu mbali mbali, na kutengenezwa maalum kwa ajili ya hospitali inayotembea ili kutoa msaada wa matibabu kwa nchi mbali mbali barani Afrika.
Mercy Ship haipo ya Afrika pekee, zipo 4 duniani ikiwemo ya kwenda visiwa vya Caribean, ya kwanza kabisa kuanzishwa inayoitwa 'Anastasis' na Good Samaritan ambayo pia ilikuwa ikizunguka duniani.
Kwenye meli hii kuna timu ya madaktari bingwa zaidi ya 450 waliotoka nchi tofauti tofauti duniani, ambao wamekuwa wakifanya miujiza kwa kubadilisha maisha ya watu ambao pengine walikuwa wameshakata tamaa, na kuwapa tumaini jipya na kujiona ni miongoni mwa jamii inayoishi.
Mpaka sasa meli hiyo imeshafanyia upasuaji zaidi ya watu 84,000 Barani Afrika kwenye nchi tofauti tofauti ikiwemo Benin, Togo, Camerron na nyinginezo, na bado inaendelea kutoa huduma hizo, ikiwemo kunyoosha miguu ya watu mbali mbali ambao waliamini kuwa ni walemavu kwa maisha yao, na kuokoa maisha ya watoto ambao hali zao walikuwa kwenye hatari ya kufa bila gharama yoyote ya matibabu.







