Alhamisi , 27th Oct , 2016

Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI leo ameondoka Jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mfalme wa Morocco Mohamed VI mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam.

 

Katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI ameagwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliyewasili nchini tarehe 23, Oktoba kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na pia viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mtukufu Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi hapa nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mgeni wake Mfalme wa Morocco Mohamed VI aliyemaliza ziara yake ya kikazi na kuondoka jijini Dar es Salaam Oktoba 27, 2016